UUNDAJI WA MANENO.

  

Uundaji wa maneno ni ujenzi au uzalishaji au utengenezaji wa maneno mapya. Uundaji wa maneno mapya husaidia kuongeza msamiati katika lugha ili kukidhi mahitaji ya mawasiliano. Uundaji wa maneno mapya husababishwa na mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni na maendeleo ya kisayansi yanayotokea katika jamii. Kwa mfano tunayo maneno mapya, kama vile ufisadi, uwekezaji, ukeketaji, ujasiriamali na mengine mengi kutokana na mabadiliko ya kijamii.

Kutumia Uambishaji

Kubainisha Mofimu katika Maneno

Bainisha mofimu katika maneno

Uambishaji wa maneno ni kitendo cha kupata maneno kwa kubandika Mofimu kwenye kiini cha neno, uambishaji kutokea kabla ya kiini cha neno au mzizi wa neno. Mfano kiini pig- unaweza kuunda maneno kama inapiga, anayepiga, mpigaji, amepigika nk.

Mofimu zinazobadilika kwenye kiini cha neno huitwa Viambishi.

Katika lugha ya Kiswahili viambishi hutokea kabla na baada ya kiini cha neno.

Mfano

Wanapendana = Wa-na-pendan-a kiini cha neno ni-pend-.

Mofimu zilizobadilisha baada ya kiini –an-na-a viambishi vinavyotokea kabla ya kiini cha neno huitwa viambisha awali au tangulizi. Viambisha vinavyotokea baada ya kiini cha neno huitwa viambishi tamati au fuatishi.

Example 1

Angalia mifano ifuatayo:

Neno Viambisha Awali Kiini Viambisha Tamati
Unapendelea u-na- -penda- el-e-a
Waliongozana wa-li- -ongoz- an-a
Analima a-na- -lim- -a
anayeiimbisha a-na-ye -imb- -ish-a

Dhima za Mofimu

Bainisha dhima za mofimu

Baadhi ya dhima za uambishaji ni kama ifuatavyo:

  1. Kuonyesha upatanisho wa usanifu maana ya maneno yanayozalishwa kutofautiana katika msingi wa kusanifu tu, lakini uhusiano wa maneno hayo hutokana na kiini au mzizi wake uleule.Mfano;Fundisha kiini chake ni fund. Unaweza kuzalisha maneno mengine kwa kutumia mzizi/kiini kilichopo kama vile fundishana, mafundisho, mfundishaji, fundishwa, fundishana.
  2. Uambishaji huonyesha nafsi
  3. Uambashaji huonyesha njeo (muda)
  4. Uambishaji huonyesha urejeshi
  5. Uambishaji huonyesha ukanushi
  6. Uambishaji huonyesha hali mbalimbali za kitenzi

Vitenzi vikiambishwa huweza kujenga/kuunda/kuzalisha vitenzi vingine au nomino.

Example 2

Mfano

Vitenzi Kiini Nomino Vitenzi
Cheza -chez- Mchezaji, mchezo wanacheza/atamchezea
Piga -pig- Mpigaji, Mpiganaji watanipiga, aliyempiga/wanaompiga

Uambishaji hutumika kuzalisha viwakilishi na vielezi.

Neno (Kiwakilishi) Kiini Kielezi
Huyu, Huyo Hu Humu, humo
Wangu, wako, wake wa
Hii, hizo, hiki hi

Viambishi awali vina dhima ya kudokeza nafsi, njia, idadi urejeshi na ukanushi.Mfano: Hawakulima

  • Ha-, kiambishi cha ukanushi
  • Ku-, kiambishi njeo/wakati

Viambishi tamati vina dhima mbalimbali hudokeza hali ya utendekaji, ukamilishaji au kimalizio cha neno na kauli za matendo kama vile kutendwa, kutendewa,kutendeka nk.

Dhima:Ukanusho, kutendeana, agizo na mtendwa, ukamilisho, usababishi.

Example 3

Mfano

Neno Viambishi Tamati
Anapiga -a
Wanapigana -an
Asipigwe -w
Amempigisha -ish-

Viambishi tamati vina dhima ya kutambulishwa mapema/nomino zilizoundwa kutokana na vitenzi.

Neno Kiini Viambishi Tamati
Piga pig- -o
Mchezo chez- -o
Mtembezi tembe- -z-i
Mfiwa -fi- -us-a

By Marco Raphael.

4 thoughts on “UUNDAJI WA MANENO.

  1. Watanzania ni watumiaji wa lugha ya kiswahili endapo kiswahili kikiondolewa watashindwa kukamilisha mawasiliano je ni madhara gani mengine atapata?

    Liked by 1 person

    1. Ndugu Ajuaye shonde

      Kwanza salamu kwako najua umesubiri kwa muda mrefu bila kupata jibu juu ya swali lako hapo juu lihusulo madhara yatakayo patikana endapo kiswahili kitaondolewa. Kwanza samahani kwa usumbufu kwa subira yako kwa muda mrefu na hii yote ni kwa sababu ya majukumu mbalimbali ya kijamii

      1. Kusaidia kuleta umoja wa taifa zima.

      2. Kudumisha utamaduni wa kitanzania kuliko kufuata kasumba.

      3. Kufanya Watanzania waamini zaidi mambo yao kuliko kutegemea tu ya kigeni.

      4. Kurahisisha upatikanaji wa ajira kwa watumiaji wa lugha hiyo hata nje ya Tanzania .

      5. Kukuza sekta ya utalii.

      Liked by 1 person

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.